AfyaMtandao

Mikataba zaidi ya Huduma za Afya yasainiwa Tanzania

Tangu kusainiwa kwa mkataba wa kwanza wa utoaji Huduma za afya kati ya Halmashauri ya Lushoto na Hospitali ya Kilutheri ya Bumbuli (2008), Halmashauri zaidi zimeingia katika mikataba na vituo binafsi vya afya ili kutoa Huduma bora na nafuu hasa kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Tayari halmashauri 37 zimeishaingia katika mikataba ya utoaji wa Huduma za afya na vituo binafsi ili kutoa Huduma za afya kwa jamii na katika hali ya ushirikiano.

Maendeleo haya kwa upande mmoja yamechangiwa na jitihada za serikali na wadau binafsi lakini pia kutokana na mafanikio ya kiafya yaliojionyesha kutokana na mkataba hasa katika kuongeza upatikanaji wa Huduma bora za afya pale ambapo mikataba hii inafanya kazi.

Ingawa changamoto chache zipo katika utekelezaji wa ushirikiano huu, faida zinabaki kuwa kubwa zaidi, vifo vya kina mama, watoto wachanga chini ya miaka mitano vimeonyesha muelekeo wa kupungua sehemu ambazo mikataba hii ipo.

Katika juhudi zilizochukuliwa katika kuboresha mazingira ya utendaji wa mikataba ya utoaji wa Huduma za afya ni pamoja na mapitio ya mwongozo wa Mipango ya Afya ya Halmashauri (CCHPII) na hasa katika eneo la utoaji wa fedha.

Vile vile kuna mpango wa serikali pamoja na washirika wake kupitia mkataba wa utoaji wa Huduma za afya na kurekebisha maeneo ambayo yamekuwa vikwazo ili kuboresha utekelezaji kwa manufaa ya uma.

 

Views: 327

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service