AfyaMtandao

Awamu ya pili ya mradi wa tunajali

Tume ya Kikrsito ya Huduma za jamii yaani Christian Social Services Commission (CSSC), kwa kushirikiana na Kampuni ya Deloitte Consulting Ltd, imeanza utekelezaji wa programu maalamu inayolenga kujumuisha matibabu ya ukimwi na programu imarishi kwa lengo la kutoa Huduma na matibabu bora yanyolingana na thamani ya fedha za wafadhili.


Mradi huo unaojulikana TUNAJALI awamu ya pili, mradi ambao unaimarisha Huduma kwa kuwajengea uwezo wa uelewa, ufahamu na kiutendaji juu ya upatikanaji wa afya bora katika jamii. Progamu hii inayotekelezwa katika wilaya zote za mikoa ya Dodoma, Iringa, Morogoro na Singida. Tume, inafanya kazi kubwa kama mbia katika utoaji wa Huduma ya kitaalamu huku Kampuni ya Deloitte Consulting Ltd ikiwa ni mbia mkuu.


Lengo ni kuziwezesha halimashauri zote ishirini na nne katika mikoa hiyo minne kupanga, kuratibu na kutoa matibabu na Huduma bora na endelevu ya ukimwi inayozingatia jinsia na usawa. Awamu hii ya pili ya TUNAJALI ina maana ya “We Care” na inaendeshwa kwa msaada wa mpango wa dharura wa ukimwi wa Rais wa Marekani, yaani U.S President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PERFAR) kupitia shirika la misaada la watu wa marekani (USAID), kwa jumla ya dola za kimarekani 680,780.00 kwa mwaka wa kwanza. Pia unalenga kutoa Huduma mathubuti na endelevu za kliniki na Huduma za ukimwi katika jamii kwa mpango maalumu kwenye vituo vya afya.

Views: 412

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service