AfyaMtandao

CSSC yazindua mpango wa kuwarejesha katika matibabu watu wanaoishi na VVU jijini Mwanza

Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii (Christian Social Services Commission) CSSC, imezindua mpango maalum wa kuwarudisha watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika huduma endelevu za matibabu ya VVU katika jiji la Mwanza.
 
Mpango huo unajulikana kama "Back To Care Initiative" umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
 
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkazi wa Centres for Disease Control & Prevention (CDC) Dr Michelle Roland unalenga kurejesha zaidi ya waVVU 8,000 ambao wameacha matibabu kwa sababu mbalimbali kama vile kujisikia vizuri, kunyimwa ruhusa kutoka kwa waajiri wao, kukosa gharama za usafiri n.k. Aidha wanaoacha matibabu ni pamoja na watoto wapatao 1600 sawa na asilimia 18 wenye umri chini ya miaka 15.
 
Madhara yanayotokana na kuacha huduma hizi ni pamoja na kuzorota afya za waVVU na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo
 
Mpango huu ambao utajumuisha wilaya za Nyamagana, Magu na Geita, utasaidia kuwawezesha watu waVVU kurejea kwenye huduma endelevu na kauli mbiu ni TIBA NI HAKI YAKO...RUDI KWENYE TIBA LEO!
 

Views: 410

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service