AfyaMtandao

AfyaMtandao kuhamasisha zaidi matumizi ya TEHAMA

AfyaMtandao kuhamasisha zaidi matumizi ya TEHAMA

Tume ya Kikristu ya huduma za jamii (CSSC) kupitia kitengo cha AfyaMtandao imepanga kujikita zaidi katika kuhamasisha matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika hospitali za taasisi za dini na zile za binafsi ambazo zipo tayari kutumia teknolojia hiyo.

Katika mpango kazi wake wa mwaka 2012, AfyaMtandao imepanga kuwa na warsha za uhamasishaji kwa wadau wa afya wa vituo mbalimbali vya afya vinavyomilikiwa na taasisi za dini, binafsi na zile za umma kuhusu umuhimu wa kutumia teknolojia ya Kompyuta katika kutoa Huduma.Warsha hizo zitajadili jinsi mifumo ya Kompyuta ya AfyaPro na Care 2X  inavyofanya kazi katika hospitali ambazo tayari zinatumia mifumo hiyo, ili kuvutia vituo vingine vya afya ambavyo havijaanza kutumia mifumo hiyo vijiunge na mifumo hiyo.

Warsha hizo za uhamasishaji zitafanyika katika kanda ya ziwa na kaskazini ambazo ndiyo mifumo hiyo inafanya kazi katika hospitali nyingi na hivyo kurahisha utoaji wa huduma ambayo inaondoa foleni kwa wagonjwa kusubiri sana ili wapate huduma.

Mbali na warsha hizo pia AfyaMtandao, imepanga kuwaunganisha wataalamu wa sekta ya afya ambao ni madaktari, wauguzi na watendaji wengine wa sekta hiyo kupitia jukwaa la majadiliano. Jukwaa hilo litatumika kwa  wataalamu hao katika kushirikishana ujuzi na uzoefu wa taaluma yao.

Pia AfyaMtandao imedhamiria kuwaunganisha wanafunzi wa taaluma ya udaktari na kuwafanya wawe karibu. Kwa kuona hilo imepanga kuwa na mtandao ambao utawahusisha wanafunzi hao wa vyuo vikuu ili waweze kushirikishana taaluma na umuhimu wa kutumia TEHAMA katika hospitali. Kwa njia hii wadau hawa watakuwa na uzoefu wa kutosha wa Teknolojia hii ya Kompyuta.

Pamoja na mkakati huo, shughuli zingine ambazo zimepangwa katika mpango kazi huo ni, kutengeneza makala za filamu zitakazoelezea umuhimu wa Teknolojia ya habari katika sekta ya afya, na jinsi teknolijia hiyo ilivyoboresha Huduma ya afya kwa hospitali na vituo vya afya ambavyo tayari vinatumia teknolojia ya Kompyuta. Kitengo cha AfyaMtandao, CSSC kimeanza mwaka 2008, kikiwa na lengo la kuboresha huduma za afya kwa vituo vya afya vilivyo chini ya  taasisi za dini kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).

 

Views: 439

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service