AfyaMtandao

Ufinyu wa Rasilimali tishio kwa afya nchini

Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa afya Jamii Dk. Seif Rashidi, amekiri kuwa ufinyu wa rasilimali bado unaendelea kuwa tishio kwa Huduma za afya nchini licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali.Dk. Rashidi aliyaeleza hayo wakati akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa 75 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) unaofanyika jijini Dar es salaam.

“Kwa hakika hii ni changamoto si tu kwa hospitali na vituo vya mashirika ya dini, bali hata kwa vituo na hospitali za umma alisema. Alisema wakati kuna vituo vingi visivyokuwa na wahudumu wenye sifa, hata vifaa vya kuendeshea vituo hivyo fedha hazitoshelezi.

“Hivyo ni imani yangu kuwa mijadala mtakayoendesha katika mkutano huu, mtajaribu kutafuta suluhisho na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tutapata busara ya kuendesha Huduma hizi” alisisitiza.

Mwenyekiti wa TCMA Dk. Isaya Tosiri alisema mkutano wao wa mwaka huu, umelenga kujadili kwa kina mada kuu mbili zitakazoleta tija zaidi katika utoaji wa Huduma zao.

“Ugonjwa wa tezi Dume utakuwa ni mada ya kwanza tutakayojadili, ambayo tumeipa siku yake maalumu, hapo tutazungumzia kwa mapana ili kuona ni kwa jinsi gani kama wataalamu tunaweza kupambana nao alisema.

Hivyo aliwataka wanaume waweze kupima afya zao mara kwa mara, ili kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa huo.

Dk.Tosiri alitaja mada ya pili itakayojadiliwa katika mkutanao huo kuwa ni jinsi ya kuendesha Huduma za afya katika mazingira magumu.

Zaidi ya madaktari wa kikristo 300 pamoja na wadau wa sekta ya afya wapo jijini Dar es salaam kushiriki maadhimisho hayo huku wakiendesha mijadala kadhaa kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya afya nchini.Mkutano huo pia unaambatana na maonyesho ya vifaa vinavotumika katika sekta ya afya.

 

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

 

 

Views: 185

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service