AfyaMtandao

CSSC yashinda Tuzo ya SADC kutambua mchango wa mashirika ya dini katika masuala ya jinsia

Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) imeshinda Tuzo ya kutambua mchango wa mashirika ya dini katika kuwawezesha wanawake kutambua haki ya afya ya uzazi. Tuzo hiyo imetolewa na Shirika linalotetea  masuala ya jinsia (Gender links) ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.

CSSC ilitangazwa mshindi na kukabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa kilele cha mkutano mkuu wa masula ya jinsia ya ukanda huo uliofanyika nchini Afrika ya Kusini. Mashindano hayo yalihusisha washiriki 213 kutoka nchi 13 ambazo ni wanachama wa SADC, na CSSC iliibuka mshindi katika kupengele cha mashirika ya dini na kuwashinda wengine 13 katika kipengele hicho.

Ushindi wa CSSC umepatikana baada ya kuwasilisha makala ya filamu (Documentary) kuhusu namna ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa  kabla ya miezi tisa (Pre-mature) kukua na kuongezeka uzito unaostahili kwa kutumia njia ya asili maarufu kama “Kangaroo method” Njia hii inatumika katika hospitali ya wilaya ya Sengerema inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita.

 

Views: 323

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

Comment by Dafroza Vicent Mabulla on May 9, 2013 at 14:08

Pongenzi kwa uongozi wa CSSC na dada Rechel kwa kutuwakilisha katika tuzo hiyo.Big Up

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service