AfyaMtandao

Hospitali Teule ya Muheza na mfumo wa Kompyuta kwa watumishi (HRIS)

Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii (CSSC) kanda ya mashariki imetoa vifaa na kufunga mfumo wa kuhifadhi taarifa za watumishi kwa njia ya Kompyuta ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za watumishi na kuwezesha menejimenti ya hospitali kupanga na kutoa maamuzi yahusuyo watumishi kulingana na taafifa hizo.

Kabla ya kufungwa mfumo huo hospitalini hapo, watumishi walipewa mafunzo jinsi ya kutumia mfumo huo katika kuweka taarifa za watumishi lakini pia kutengeneza ripoti kulingana na idadi ya watumishi wa kada mbalimbali walioingizwa katika mfumo huo.

Akitoa maelezo kuhusiana na mfumo huo, Katibu wa kanda ya mashariki Dk. Narcisius Kibozi, amesema, kufungwa kwa mfumo huo katika hospitali Teule ya Muheza kutaboresha na kutarahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za watumisha, hivyo kuwasidia katika kupanga mipango mbalimbali kuhusu watumishi  kama vile ratiba ya kwenda likizo, mafunzo na hata upandishwaji wa madaraja.

Vifaa vilivyotolewa katika kufunga mfumo huo ni pamoja na, Kompyuta, Monitor, scanner, printer na kifaa kinachounganisha mfumo huo kijulikanacho kama Appliance.
Katibu wa Tume ya kikristu Kanda ya Mashariki Dr. kibozi akiongea na uongozi wa hospital kuhusu umuhimu wa HRIS na matumizi yake

Views: 604

Add a Comment

You need to be a member of AfyaMtandao to add comments!

Join AfyaMtandao

© 2024   Created by sona.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service